IQNA

Mkutano wa "Mashambulizi Dhidi ya Gaza, Kulengwa Baitul Muqaddas" wafanyika Palestina

9:58 - February 04, 2009
Habari ID: 1739989
Mkutano wa Mashambulizi Dhidi ya Gaza, Kulengwa Baitul Muqaddas" umefanyika katika mji mtukufu wa Baitul Muqaddas, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Qadhi Mkuu wa Palestina Sheikh Taysir al Tamimi alihutubia mkutano uliohudhuriwa na mamia ya watu akisisitiza kuwa ulimwengu unapaswa kuchukua hatua za haraka za kuokoa matukufu ya Kiislamu na Kikristo.
Kuhusu hitilafu za makundi ya Kipalestina, Sheikh al Tamimi amesema, mivutano hiyo inaifaidisha Israel pekee na kuusaidia utawala huo wa Kizayuni kufikia malengo yake ya kuikalia kwa mabavu na kuiharibu Palestina kwa wepesi.
Kwa upande wake Mwenekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Baitul Muqaddas Sheikh Ikrima Sabri amesema kuwa uchimbaji unaofanywa na Israel chini ya msikiti wa al Aqsa unatishia utambulisho, historia na ustaarabu wa Kiislamu.
Sheikh Sabri amemshukuru Waziri Mkuu wa Palestina Recep Tayyip Erdogan kwa kuwatetea Wapalestina katika kikao cha Davios Uswisi na akasema, katika kipindi cha sasa ambapo kadhia ya Baitul Muqaddas imesahaulika kutokana na jinai zilizofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, zinapaswa kufanyika juhudi kubwa za kulilinda eneo hilo tukufu.
Sheikh Ikrima Sabri ameashiria uharibifu uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya shule ya Umoja wa Mataifa kutokana na uchimbaji unaofanywa na utawala huo katika msikiti wa al Aqsa na akasema: UNISEF inapaswa kufanya jitihada kubwa za kulinda maeneo matukufu ya Kiislamu. 358708
captcha