Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Jumuiya ya Sinema ya Vijana wa Iran, Nasser Bakideh katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watengeneza Filamu Fupi wa Nchi za Kiislamu ameongeza kuwa: “Tamasha hiyo inakusudia kuimarisha fikra ya mapambano endelevu ya Wapalestina na kuwasilisha taswira ya kweli kuhusu matukio halisi ya ardhi hiyo. Aidha inakusudia kuarifisha mapambano na namna Wapalestina walivyodhulumiwa”.
Bakideh ameongeza kuwa tamasha hiyo ya filamu pia itafayika wakati mmoja katika nchi za Lebanon, Sudan na Algeria mwezi Mei mwaka 2009.
Tamasha hiyo ya filamu imeandaliwa kwa himaya ya Jumuiya ya Sinema ya Vijana wa Iran, Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran, na Kamati ya Ofisi ya Rais wa Iran kwa ajili ya kuunga mkono mapambano ya Palestina na idara za utamaduni za Iran mjini Beirut na Khartoum.
Amesema, tamasha ya kwanza ya “Ardhi ya Zaitun" itajumuisha kitengo cha filamu fupi,mswada filamu na picha.
Watengeneza filamu wapiga picha na waandishi wa miswada ya filamu wanaweza kuwaslisha kazi zao kuhusu maudhui kama vile; dhulma, hali ya Palestina kwa mtazamo wa haki za binadamu, mashahidi wa Intifadha, nafasi ya wanawake katika intifadha na mchango wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika mapambano ya Palestina. Washiriki wanaweza kutuma kazi zao kwa anuania ifuatayo:
Iran Short Film Makers Association Vanak Square, South Gandi, Alley 19 No. 20 Tehran, Iran 358891