IQNA

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuunda kamati ya kufuatilia jinai za utawala wa Kizayuni

10:43 - February 07, 2009
Habari ID: 1741056
Mahmoud Rashid Ghalib, Mkuu wa Idara ya Sheria ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa jumuiya hiyo itabuni kamati ya kufuatilia jinai zilizotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Hayo yamesemwa na Shirika Rasmi la Habari la Imarati WAM ambalo limeongeza kuwa, katika hali ya hivi sasa Amr Musa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu anafanya juhudi za kutafuta watu wanaofaa wa kimataifa na wa kutegemewa watakaoorodheshwa kwenye kamati hiyo.
Mahmoud Rashid Ghalib amesema kuwa, kufuatia mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imefanya vikao kadhaa vya kukusanya ushahidi wa jinai za kivita kwa ajili ya kuwashtaki watawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Ghalib ameongeza kuwa, mara tu baada ya kukamilika wanachama wa kamati hiyo, ushahidi na mitazamo yao itachunguzwa katika kikao cha dharura huko Cairo kwa madhumuni ya kuwasilishwa mashtaka dhidi ya wakuu wa utawala haramu wa Israel katika mahakama iliyotajwa.
Mkuu huyo wa Idara ya Sheria ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, kamati hiyo ambayo ni ya kwanza ya aina yake kuundwa na jumuiya hiyo, itasafiri hadi Gaza kwa ajili ya kukusanya ushahidi zaidi kuhusiana na jambo hilo. 360264
captcha