IQNA

New York Times: Waarabu waliisaidia Israel katika vita vya Gaza

14:05 - February 07, 2009
Habari ID: 1741265
Gazeti la Kimarekani la New York Times limemethibitisha kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu ziliusaidia utawala ghasibu wa Israel wakati wa mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Shirika rasmi la Habari la Syria SANA limeripoti kuwa New York Times limeandika: Nchi za Kiarabu waitifaki wa Israel ziliusaidia utawala huo katika vita vya siku 22 dhidi ya Ukanda wa Gaza na kwamba Uturuki ilipinga mipango yote ya Israel kuhusu vita hivyo.
Gazeti hilo limeashiria hotuba ya Waziri Mkuu wa Uturuku Recep Tayyep Erdogan katika mkutano wa kiuchumi wa Davos na kuandika kuwa: Vita vya Gaza vimevuruga uhusiano wa Uturuki na Israel ambao umeharibika zaidi baada ya hotuba ya Erdogan katika mkutano huo.
New York Times limesisitiza kuwa mtazamo wa Uturuki unatofautiana kikamilifu na ule wa Israel kuhusu harakati ya Hamas na kuandika kuwa: Ankara inaitambua Hamas kuwa ni harakati ya kidemokrasia inayoungwa mkono na wananchi huku Tel Aviv ikidai kwamba harakati hiyo ni kundi la kigaidi. 360244
captcha