IQNA

Mwendesha Mashtaka wa Uturuki ataka jinai za Wazayuni Gaza zichunguzwe

10:03 - February 09, 2009
Habari ID: 1741727
Mwendesha Mashtaka wa Uturuki ameanza kufanya uchunguzi kuhusu jinai za Israel dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na utawala huo haramu dhidi ya watu wa Gaza.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Islamonline, uchunguzi huo umeanza baada ya Jumuiya ya Haki za Binaadamu ya Uturuki kuchukua jukumu la kufuatilia jinai za Wazayuni huko Gaza.
Katika ombi lake kwa mahakama, mwendesha mashtaka huyo anataka viongozi 19 wa utawala haramu wa Israel wakiwemo Rais Shimon Peres, Waziri Mkuu Ehud Olmert, Waziri wa Mambo ya Nje Tzipi Livni na Waziri wa Vita Ehud Barak wahukumiwe kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari na jinai za kivita huko Gaza.
Kwa mujibu wa sheria za Uturuki, mahakama za nchi hiyo zina uwezo wa kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya watenda jinai za mauji ya kimbari na kivita popote walipo duniani.
Itakumbukwa kuwa katika vita vya siku 22 vya Wazayuni dhidi ya Gaza vilizoanza Disemba 27 mwaka 2008, Wapalestina wasiopungua 1300 waliuawa shahidi nusu yao wakiwa wanawake na watoto. Watu wengine zaidi ya 5000 walijeruhiwa huku mamia ya maelfu wakiachwa bila makazi.
Utawala wa Kizayuni pia ulitumia silaha za sumu katika hujuma yake mbali na kuhujumu shule, misikiti na mahospitali. 360511



captcha