IQNA

Cairo kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu

11:43 - February 10, 2009
Habari ID: 1742331
Mkutano wa 21 wa kimataifa wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu unatazamiwa kufanyika tarehe 5 mwezi ujao wa Machi mjini Cairo, Misri.
Gazeti la al Watan la Saudi Arabia limeripoti kuwa mkutano huo utakaosimamiwa na Rais Hosni Mubarak wa Misri utaendelea hadi tarehe saba Machi.
Wawakilishi wa nchi 95 za Kiarabu na zisizokuwa za Kiarabu na jumuiya kadhaa za kimataifa watashiriki katika mkutano huo wa 21 wa kimataifa wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu. 361266
captcha