IQNA

Kufungamana na Mosad sababu ya kimya cha baadhi ya serikali mbele ya jinai za Israel

12:13 - February 10, 2009
Habari ID: 1742336
Uhusiano wa baadhi ya nchi za Kiislamu na shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mosad, ndio sababu kuu iliyozipelekea nchi hizo kukaa kimya kuhusiana na jinai zilizotekelezwa hivi karibuni na utawala huo haramu dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Akizungumza hivi karibuni katika kikao cha ‘Mfungamano na Watu wa Gaza' kilichofanyika mjini Karachi Pakistan, Qasir Bangali, mwandishi na mchanbuzi mashuhuri wa masuala ya kisiasa wa nchi hiyo amesema kuwa, shirika la ujasusi la utawala wa Israel Mosad, limekuwa likitoa habari za siri za wapinzani wa watawala wa nchi za Kiislamu na hivyo kuwafanya wafungamane na kulitegemea shirika hilo ili kuendelea kubaki madarakani.
Amesema, jambo hilo limewapelekea watawala hao kukaa kimya mbele ya jinai na mauaji ya umati yaliyotekelezwa hivi karibuni na utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza, katika hali ambayo raia wa kawaida wa nchi hizo walitoka mitaani na kulalamikia vikali jinai hizo.
Bangali amesema kuwa, nchi zilizonyamazia kimya jinai hizo bila shaka ni washirika wakubwa wa watenda jinai hizo. 361309
captcha