Shirika la habari la kimataifa la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu IINA rimepoti kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho Alexander Faiger amesema, masomo kituoni hapo yatatolewa kwa lugha ya Kijerumani na kwamba hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa wahubiri na maimamu wa misikiti ya Ujerumani kupata masomo ya Kiislamu kwa lugha ya Kijerumani.
Amesema kuwa vijana wa Kiislamu wakataohitimu masomo katika kituo hicho watafunza masomo ya Kiislamu katika shule za Ujerumani au kufanya kazi misikitini kama maimamu wa swala za jamaa.
Alexander Faigar ameashiria kwamba kituo hicho cha kutoa mafunzo kwa maimamu wa misikiti kinasubiri kusajiliwa rasmi na taasisi husika za serikali na kuongeza kuwa awali kitapokea wanafunzi 32 wa Kiislamu ambao watapewa mafunzo kwa lugha ya Kijerumani.
Hadi sasa shahada za kuhitimu masomo ya uimamu na kulingania Uislamu hazikuwa zikitambuliwa rasmi na serikali ya Ujerumani.
Hii ni mara ya kwanza kwa kituo cha mafunzo ya maimamu wa misikiti kupata kibali rasmi cha Wizara ya Elimu ya Ujerumani. 362176