IQNA

Mbunge mwenye misimamo ya kupindukia mipaka wa Uholanzi azuiwa katika uwanja wa ndege mjini London

12:23 - February 14, 2009
Habari ID: 1743617
Geert Wilders, mbunge mwenye misimamo ya kupindukia mipaka wa Uholanzi aliyetengeneza filamu iliyo dhidi ya Uislamu iitwayo Fitna, amezuiwa kuingia nchini Uingereza akiwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London, na hatimaye kurejeshwa nchini kwake.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imesema kuhusiana na suala hilo kwamba, awali mbunge huyo alikuwa amefahamishwa na serikali ya London marufuku iliyokuwepo dhidi yake kuingia nchini Uingreza lakini alipuuza tahadhari hiyo na kusafiri nchini Uingereza bila ya kuwa na kibali.
Msemaji wa wizaya hiyo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria za Uingereza, kila mtu anayeingia nchini humo bila ya kuwa na kibali rasmi anapaswa kukamatwa na polisi ya nchi hiyo na kurejeshwa nchini kwake kama alivyofanywa Wilders.
Serikali ya Uholanzi imebainisha masikitiko yake kuhusiana na kitendo hicho cha polisi ya Uingereza dhidi ya mbunge wake.
Inakumbushwa hapa kuwa, Wildres alialikwa nchini Uingereza na Lord Pearson kwa ajili ya kuonyesha filamu ya Futna iliyojaa matusi dhidi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu katika Bunge la Wazee (House of Lords) la Uingereza lakini ubalozi wa nchi hiyo mjini The Hague ulimnyima viza ya kusafiria ukisema kuwa filamu yake hiyo ilikusudia kuchochea hisia za kidini na hivyo kuvuruga amani na utulivu wa jamii ya Uingereza, jambo linalopingwa vikali na serikali ya nchi hiyo.363339
captcha