Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Watan, tovuti hiyo itawawezesha Waislamu kufahamu maduka yanayouza bidhaa na vyakula halali vinavyooana na mafundisho ya dini yao na ambavyo havipingani na sheria za Kiislamu.
Katika siku ya kwanza ya kuzinduliwa tovuti hiyo, orodha ya majina ya mashirika 120 yanayozalisha bidhaa na vyakula halali vya watoto na vya kuganda nchini Ujerumani yaliorodheshwa. Mashirika hayo huchinja wanyama kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na pia kutoweka nyama ya nguruwe katika orodha ya nyama zinazouzwa na maduka hayo.
Kwa kurejea katika tovuti hiyo, watu walio na hamu ya kununua vyakula hivyo wanaweza kufahamu namna vyakula hivyo vinavyotengenezwa na pia kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na vyakula vyenye afya kwa mwili wa mwanadamu.363350