Gazeti la Statement la Kolkata Alhamisi iliyopita lilichapisha makala inayoivunjia heshima dini ya Kiislamu ambayo ilipewa anwani ya "Kwa nini tunapaswa kuziheshimu dini za Kidikteita?", suala ambalo limekabiliwa na malalamiko makali ya Waislamu na vyama vya Kiislamu nchini India.
Makala hiyo ambayo awali ilichapishwa katika gazeti la Indipendent la Uingereza tarehe 5 Februari, imezungumzia mambo machafu yanayouvunjia heshima Uislamu na kuwakasirisha wafusi wa dini hiyo.
Baada ya makala hiyo kuchapishwa tena katika gazeti la Statement, Waislamu wa mji wa Kolkata nchini India walikusanyika mbele ya jengo la gazeti hilo na kuwasilisha mashkata mahakamani dhidi ya mwandishi wa makala hiyo.
Polisi ya Kolkata imetangaza kuwa imemtia nguvuni mwandishi wa Statement kwa tuhuma za kuzusha fitina na mapigano ya kikaumu na kidini na kuchochea hisia za Waislamu. 363372