IQNA

Njia za kisheria za kuhukumiwa watawala wa Israel zaandaliwa

18:43 - February 17, 2009
Habari ID: 1745364
Ujumbe wa Palestina ukiongozwa na Riadh al-Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina umekutana jana Jumatatu na Lius Moreno Ocampo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa lengo la kuchunguza njia za kisheria za kuhukumiwa watawala wa Israel waliohusika na jinai za kivita dhidi ya watu wasio na hatia huko katika Ukanda wa Gaza.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe huo wa Palestina uliwasilisha nyaraka za kuaminika za jinai zilizofanywa na watawala hao wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina wakiwemo watoto na wanawake wasio na hatia.
Riadh al-Maliki amesema Katika mazungumzo hayo kuwa, bado hatua nyingine zinachukuliwa kwa lengo la kuwashtaki watawala wa kisiasa na kijeshi wa utawala haramu wa Israel katika mahakama ya ICC kutokana na jinai walizotenda dhidi ya binadamu.
Akizungumzia suala hilo, Ali Khashan, Waziri wa Sheria wa Palestina pia amesema kuwa kuna taasisi na mashirika mengi ya kisheria ya Kiarabu na ya kimataifa yaliyowasilisha mashtaka kama hayo dhidi ya watawala wa Kizayuni katika mahakama hiyo ya kimataifa. 365278
captcha