IQNA

Papa apanga kukutana na viongozi wa Kiislamu wa Jordan

12:19 - February 19, 2009
Habari ID: 1745835
Papa Benedict wa XVI wa Kanisa Katoliki Duniani anapanga kukutana na viongozi wa Kiislamu wa Jordan atakapofanya safari nchi humo mwezi Mei mwakani.
Katika mazungumzo yake na viongozi hao yaliyopangwa kufanyika katika msikiti wa Mfalme Hussein mjini Amman, Papa Benedict amepanga kujadiliana nao kuhusiana na umuhimu wa kufanyika mazungumzo kati ya dini mbili muhimu za Kiislamu na Kikristo. Nafasi ya dini katika kueneza amani na uadilifu ulimwenguni na hasa katika eneo la Mashariki ya Kati ni maudhui ziliyopangwa kupewa umuhimu katika mazungumzo hayo.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2006 Papa huyo huyo aliamsha hasira kubwa ya Waislamu alipotoa matamshi ya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kwa kudai kwamba Uislamu ni dini inayotumia mabavu. Tokea wakati huo, Papa huyo amekuwa akifanya juhudi za kuonyesha kwamba ni mtu anayewatakia wema Waislamu na pia kuimarisha uhusiano wa Vatican na taasisi muhimu za Ulimwengu wa Kiislamu.
Wakristo wapatao laki mbili wengi wao wakiwa ni wafuasi wa Kanisa Katoliki wanaishi nchini Jordan ambayo ina idadi ya watu karibu milioni 6. 366010
captcha