IQNA

Juhudi za Sami Yusuf za kusahihisha sura ya Waislamu katika nchi za Magharibi

12:34 - February 19, 2009
Habari ID: 1745838
Sami Yusuf, muimbaji mashuhuri wa Kiislamu ameelezea masikitiko yake kuhusiana na picha potofu waliyonayo watu wa nchi za Magharibi kuhusiana na Waislamu na kusema kuwa, muziki wake ni sehemu ya juhudi za kusahihisha sura hasi iliyoenea katika nchi hizo kuhusiana na Uislamu na Waislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Bashair, Sami Yusuf amezungumzia suala hilo katika mazungumzo yake na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa, lengo halisi la muzuki wake ni kudhihirisha sura halisi ya Uislamu na Waislamu ulimwenguni. Amesisitiza kwamba yeye ni mwakilishi wa Uislamu halisi na sio wa Usama bin Laden. Ameelezea matumaini yake kwamba muziki wake utasaidia kuondoa misimamo ya kupindukia mipaka inayodhidhirishwa na baadhi ya Waislamu na kueneza moyo wa usamehevu na wepesi miongoni mwao.
Sami Yusuf ametetea muziki wake kwa kusema, sanaa yake inasisitiza suala la dini na thamani za ulimwengu na kiutu bila ya kujali tofauti za rangi, utamaduni na dini. Amesema, kamwe hana nia ya kukanyaga itikadi na thamani za Uislamu wake.
Huku akikosoa ropiti ya polisi ya New York kwamba mgogoro wa utambulisho ndio unaopelekea kudhihiri kwa vitendo vya utumiaji nguvu miongoni mwa matabaka ya vijana wa Kiislamu katika nchi za Magharibi, Sami Yusuf amesema kuwa mgongano uliopo miongoni mwa vijana wa Kiislamu wanaoishi katika nchi za Magharibi kuhusiana na thamani za Magharibi na Kiislamu ndilo jambo linalowapelekea kuchukua misimamo mikali na ya kupindukia mipaka.365778
captcha