Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic Events, katika kikao hicho ambacho kinahudhuriwa na Waislamu wa kike na kiume kutoka kila pembe ya mji wa Brussels, mji mkuu wa nchi hiyo, Rachid Haddach mwanafikra mashuhuri wa Ubelgiji atazungumza na kuchambua aya na hadithi mbalimbali za Kiislamu zinazozungumzia jinsi ya watoto wanavyopasa kupewa mafunzo na malezi na wazazi wao kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu.
Kikao hicho cha siku moja kinafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Brussels. 366759