IQNA

Usajili wa washiriki wa mashindano ya Qur'ani na Sunna waanza Saudia

9:02 - February 23, 2009
Habari ID: 1747426
Usajili wa majina ya washiriki katika duru ya saba ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani, Sunna za Mtume na Hotuba ya Muhammad bin Fahd bin Jalwi umeanza katika pembe zote za Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la nchi hiyo SPA mashindano hayo yamepangwa kuanza Jumamosi tarehe 4 Aprili. Yatafanyika katika makundi mawili ya wanawake na wanaume katika mkoa wa Ihsa. Mashindano hayo yamepangwa kuanza saa kumi na nusu kwa wakati wa Saudi Arabia katika misikiti tofauti ya mkoa huo.
Wafungwa na makundi ya wachache wanaoishi nchini humo pia yamepewa fursa ya kushiriki katika mashindano hayo kuanzia tarehe 9 hadi 10 za mwezi huohuo wa Aprili.
Ahmad bin Hamad Abu Ali, Katibu Mkuu wa mashindano hayo amesema kuwa, uandaaji na uendeshwaji wake utatofautiana na mashindano yaliyopita, na kuwa uzinduliwaji na utumiwaji wa mtandao wa intaneti ni miongoni mwa mabadiliko hayo.
Raia wa Saudi Arabia wanaweza kujua namna ya usajili, uendeshaji na ushiriki katika mashindano hayo kupitia anwani ifuatayo ya mtandao: www.musabaqa.org. 367723
captcha