IQNA

Kukariri madhambi hudhoofisha imani ya mja

10:38 - February 26, 2009
Habari ID: 1748776
Kukariri na kushikilia maasi hudhoofisha imani ya mja ya kuharibu kabisa itikadi zake.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Hussein Ansarian ambaye amesisitiza juu ya umuhimu wa kutubia madhambi harakaka baada ya kutumbukia katika maasia.
Sheikh Ansarian amesema kuwa kukariri na kung'ang'ania maasia huharibu saada ya mwanadamu na kumnyima fursa ya kutubia na kurejea kwa Mola wake. Amesema kukariri madhambi humfanya mwanadamu akane aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur'ani kwa kujua au kutojua.
Sheikh Ansarian amesema, mtu anayekariri madhambi na maasi bila ya kurejea kwa Mola na kutubia hutumbukia katika mtego wa kukana aya za Qurani, Mwenyezi Mungu, Mtume wake na siku ya Kiyama na hatimaye kufariki dunia akiwa nje ya dini.
Hujjatul Islam Walmuslimin Ansarian amesema, hatua ya kwanza ya kutubia madhambi ni kuungama madhambi hayo na kwamba awamu muhimu zaidi ya kuacha maasi ni ile ya baada ya toba ambapo mja anapaswa kuazimia haswa kuacha maasi.
Sheikh Ansarian amewausia Waislamu kuomba maghufira kwa Mola Muumba ili awafutie madhambi kabla ya kufariki dunia. 369227
captcha