IQNA

al Azhar: Kitendo cha Israel cha kuwavunjia heshima Mitume kinavuruga mazungumzo kati ya dini mbalimbali

11:12 - March 01, 2009
Habari ID: 1749837
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya chuo cha al Azhar cha Misri imetangaza kuwa kitendo cha televisheni ya Israel cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na Nabii Issa Masih pamoja na mama yake Bibi Maryam (as) kinaharibu mazungumzo kati ya dini mbalimbali na kitakuwa na taathira mbaya.
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar imesema kuwa hatua hiyo ya televisheni ya Israel ya kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu inazusha mivutano na ugomvi kati ya wafuasi wa dini za mbinguni.
Taarifa ya wanafikra wa al Azhar imewataka maafisa wa televisheni ya Israel kusitisha vipindi vinavyowavunjia heshima Mitume wa dini za Mwenyezi Mungu.
Taarifa hiyo pia imetahadharisha juu ya taathira mbaya za kukaririwa vitendo kama hivyo na kusisitiza kuwa kukaririwa kitendo kama hicho kutajeruhi hisia za Waislamu kote duniani.
Kanali ya 10 ya televisheni ya utawala ghasibu wa Israel wiki iliyopita ilitayarisha vipindi vilivyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw), Nabii Issa Masih na mama yake Bibi Maryam (as). Kitendo hicho kiovu kimelaaniwa na jumuiya za kimataifa na baadhi ya nchi za Kiislamu. 370341
captcha