IQNA

al Azhar kusimamia mkutano wa kimataifa wa kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu

11:01 - March 01, 2009
Habari ID: 1749843
Mkutano wa 13 wa kimataifa wa kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu unatazamia kufanyika tarehe 11 Machi katika mji wa Cairo. Mkutano huo utasimamiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya chuo cha al Azhar.
Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchango wa mivutano ya makundi mbalimbali katika kudhoofisha umma wa Kiislamu, njia za kulinda umoja na mshikamano wa Kiislamu na chuki na kidini.
Mkutano wa 12 wa kimataifa wa kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu ulifanyika mwaka 2002 na ulichunguza sababu za kihistoria za hitilafu kati ya madhehebu za Kiislamu hususan kati ya Shia na Suni.
Mkutano huo ulisisitiza juu ya udharura wa kufanyika juhudi za kuepusha hitilafu kati ya makundi ya Kiislamu na kuwasaidia wananchi wanaodhulumika wa Palestina katika mapambano yao dhidi ya hujuma za Israel. 370233


captcha