IQNA

Chuo Kikuu cha Imam Swadiq chataka kuhuisha azimio la Umoja wa Mataifa wa kufuta ubaguzi wa aina zote

10:45 - March 02, 2009
Habari ID: 1750408
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Imam Swadiq nchini Iran wamemwandikia barua Waziri wa Sheria wakimtaka kufanya juhudi za kuhuisha azimio la Umoja wa Mataifa linalosisitiza juu ya udharura wa kufutwa ubaguzi wa aina zote ambalo pia limeutambua Uzayuni kuwa ni ubaguzi wa kizazi.
Sehemu moja a barua hiyo imesema kuwa azimio nambari 3379 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambalo linafafanua aina zote za ubaguzi, tarehe 10 Novemba 1975 liliutambua Uzayuni kuwa ni ubaguzi wa kizazi, lakini kadhia hiyo imesahaulika kutokana na njama za serikali ya kibeberu ya Marekani.
Imesema kuwa kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni duniani hususan katika ulimwengu wa Kiislamu na ushindi wa wapiganaji shupavu na wenye imani wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 22 huko Gaza ambao na ushindi wa pili wa wapiganaji wa Kiislamu dhidi ya maghasibu wa Israel katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, fikra za waliowengi duniani zimesimama dhidi ya Wazayuni na waitifaki wao likiwemo Baraza la Usalama, Umoja wa Mataifa, Ulaya, Misri, Saudi Arabia na Jordan.
Barua hiyo imesisitiza kwamba kwa kuzingatia hali hiyo, Wizara ya Sheria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapaswa kutumia mashirika kama Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote kuwasilisha tena azimio hilo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuutangaza tena utawala ghasibu wa Israel kuwa ni utawala wa kibaguzi na ugaidi wa kiserikali. 370875

captcha