Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Fiqhi ya Kiislamu imesema kuwa hatua ya televisheni ya utawala haramu wa Israel ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) si ya kwanza katika uwanja huo na kwamba utawala huo una historia ya muda mrefu ya kuwakosea heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu.
Jumuiya ya Fiqhi ya Kiislamu imesisitiza kuwa, kitendo hicho ni katika mfululizo wa vitendo viovu vya Israel vya kuwatusi na kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu, Uislamu, Waislamu na matukufu yao.
Taarifa ya jumuiya hiyo imesema kuwa kitendo hicho kiovu kimezijeruhi hisia za wafuasi wa dini zote za Mwenyezi Mungu duniani na kuongeza kuwa wiki moja iliyopita kanali ya kumi ya televisheni ya Israel pia ilimdunisha na kumkosea heshima Nabii Issa na mama yake Maryam amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na jumuiya za Kiislamu na Kikristo. 371566