Amesema kuwa mikutano kama hiyo ni fursa ya kuwasilishwa mbinu bora zaidi za kiuchumi na kwamba nchi za Kiislamu zinaweza kufaidika na fursa hiyo kuboresha uchumi kwa kipindi kirefu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ameongeza kuwa siasa za jumuiya hiyo zimesimama juu ya msingi wa kustawisha zaidi hali ya kiuchumi ya nchi za Kiislamu na kuzidisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo.
Ihsanoglu ameashiria mgogoro wa kiuchumi uliozikumba nchi mbalimbali dunia na akasema, tunapaswa kuelewa kuwa mgogoro wa kiuchumi wa nchi za Magharibi umeathiri pia uchumi wa nchi za Kiislamu na kwamba nchi hizo za Kiislamu zinawajibika kuimarisha zaidi uhusiano wao wa kibiashara kwa shabaha ya kuzuia kupanuka zaidi mgogoro huo.
Mkutano huo unawashirikisha wasomi na wataalamu masuala ya kiuchumi kutoka nchi mbalimbali dunia kwa lengo ya kuchunguza mgogoro wa kimataifa wa kiuchumi na jinsi ya kukabiliana na mgogoro huo. 372195