IQNA

Benki ya Kiislamu ya Thailand kutoa msaada ya kifedha kwa Waislamu wa kusini mwa nchi hiyo

14:41 - March 07, 2009
Habari ID: 1752791
Benki ya Kiislamu ya Thailand imetenga bajeti ya baht milioni 80 kwa ajili ya kuboresha hali ya kiuchumi ya Waislamu wa kusini mwa nchi hiyo.
Mwandishi wa IQNA Asia ya Kusini ameripoti kuwa Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Thailand ameema, benki hiyo imeazimia kutoa msaada wa kifedha kwa makampuni ya Kiislamu yanayozalisha na kuuza nje bidhaa za halali. Amesema kuwa bajeti hiyo ya baht milioni 80 imetengwa kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu wa kusini mwa Thailand.
Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Thailand ameongeza kuwa fedha hizo zinaweza kusaidia juhudi za kuondoa matatizo ya kiuchumi ya Waislamu wa eneo lililobakia nyuma kimaendeleo la kusini mwa nchi hiyo. 373326

captcha