IQNA

Kinyume na wenzake, Mustafa Ismail hakuwa akishurutisha kuchukua malipo

13:38 - March 08, 2009
Habari ID: 1753148
Mustafa Ismail, msomaji mashuhuri wa Qur'ani Tukufu wa Misri alikuwa mtu mwenye nia njema na ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu, jambo lililompelekea kupata kipawa maalumu cha usamoji Qur'ani.
Alikuwa mtu mpole ambaye, kinyume na wasomaji wa Qur'ani wa zamana zake, hakushurutisha malipo katika usomaji wake wa kitabu hicho kitakatifu. Alikuwa akikataza jambo hilo na kutahadharisha dhidi ya matokeo yake mabaya kwa kusema kuwa, sharti kama hilo kwa wasomoji Qur'ani, ni msiba mkubwa.
Mustafa Ismail bila shaka alikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani nchini Misri na hasa katika upande wa kitaalamu na kisanii wa usomaji huo. Alikuwa na mbinu yake maalumu ya usomaji Qur'ani ambayo hakuiiga kutoka kwa wasomaji wengine bali yeye mwenyewe alivumbua mbinu hiyo ya usomaji, jambo lililowavutia wengi na kuwafanya kufuata na kumuiga katika usomaji huo.
Watawala wote wa Misri walivutiwa sana na usomaji wa Mustafa Ismail kiasi cha kumpa lakabu ya An'waru Sadaat. Moja ya sifa muhimu za Mustafa Ismail ni kuwa alikuwa akizingatia vyema mazingira ya wasikilizaji wake na kisha kuwasomea aya zilizonasibiana na hali pamoja na mazingira waliyokuwemo. 373765
captcha