Akizungumzia suala hilo, Abdul Aziz Hussein Ali al-Hassuni, mmoja wa wasomaji mashuhuri wa kimataifa wa Qur'ani kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu amesema katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari za Qur'ani IQNA kuwa, kila mtu anaweza kufahamu vyema na kwa urahisi maana ya aya zinazosomwa kupitia mbinu ya marehemu Mustafa Ismail.
Ali al-Hassuni amesema ili kuweka wazi zaidi maana ya aya alizokuwa akisoma Mustafa Ismail, alikuwa akisoma kwa lahani na sauti tofauti aya zilizokuwa zikihusiana na masuala tofauti kama vile ya adhabu au rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Ameongeza kuwa, licha ya kuwa Ustadh Ismail alinufaika mno na walimu mashuhuri wa Qur'ani kama vile Sha'shai na Muhammad Raf'at, lakini wakati huohuo alibuni mbinu yake mwenyewe ya usamoji Qur'ai na hivyo kuibuka kuwa msomaji mwenye kisomo chake malumu kisichoshuhudiwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani.
Amesema, lahani maalumu wa usomaji Qur'ani uliozingatiwa na Ustadh Ismail ni moja ya masuala muhimu yaliyompelekea kupata umashuhuri maalumu wa usomaji Qur'ani ulimwenguni. 373715