Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Jeffrey Feltman amewasili Beirut baada ya kutembelea Damascus na kukutana na viongozi wa Syria.
Mjumbe wa Marekani Mashariki ya Kati alitazamiwa kukutana pia na Sheikh Abdulamir Qublan, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia, Mufti wa Lebanon Sheikh Muhammad Rashid Qabbani, kiongozi wa Wamaroni Samir Nasrullah Safir na Mkuu wa kundi la Lebanese Forces Samir Jaajaa. 374806