IQNA

Mkisto aliyesilimu hivi karibuni:

Makosa ya Injili yamenihamasisha kuwa Muislamu

10:49 - March 11, 2009
Habari ID: 1754703
Makosa mengi na upotoshaji mkubwa unaoonekana kwenye kitabu cha Injili ndiyo sababu iliyonihamasisha kukubali dini ya Kiislamu. Hayo yamesemwa na Husni Mubambala, aliyesilimu hivi karibuni kutoka dini ya Kikristo.
Mubambala ambaye ametoka Uganda anashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na Hadithi yanayofanyika nchini Iran.
Amesema, kuna makosa mengi katika kitabu cha Injili na sababu yake ni kuwa kitabu hicho kiliandikwa na watu na hakikutoka kwa Mwenyezi Mungu. Amesema kuwa moja ya mambo ambayo hayawezi kukubalika katika kitabu cha Injili ni imani ya utatu mtakatifu.
Mganda huyo aliyekubali Uislamu hivi karibuni ameeleza jinsi alivyosilimu na kuongeza kuwa yeye peke yake ndiye aliyekubadili dini ya Kiislamu katika familia yake na kwamba ndugu zake wengine ni Wakatoliki.
Husni Mubambala amesema kuwa amekutana na Mawahabi wengi na kugundua kwamba misingi wanayotumia kuhalalisha na kuharamisha mambo mengi haina dalili za kimantiki na ni kwa msingi huo ndiyo maana wanawakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia ambao ni wafuasi halisi wa Mtume Muhammad (saw) na khalifa wake Imam Ali bin Abi Twalib (as).
Ameyataja mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na Hadithi yanayofanyika nchini Iran kuwa yana umuhimu mkubwa na kuongeza kuwa yanawafanya washiriki kutoka nchi mbalimbali kutambuana na kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Hafidhi huyo wa Qur'ani kutoka Uganda amesema kuwa Mawahabi waliahidi kumpa nyumba, gari, fedha na kadhalika ili ahubiri fikra za kundi hilo lakini alikataa pendekezo hilo kwa sababu fikra zao hazina mantiki.
Asilimia 45 ya wakazi milioni 30 wa Uganda ni Waislamu. 376023
captcha