Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Cameroon Said Ali Hamduo ambaye ameongeza kuwa, dini ya Kiislamu ni dini yenye misimamo ya wastani na inayopinga mwenendo wa misimamo mikali na chuki za kimadhehebu. Sheikh Said Ali Hamduo amesema kuwa aya za Qur'ani Tukufu zimekataza misimamo ya taasubi na chuki za kidini na kwamba dini ya Kiislamu imejengeka juu ya msingi wa upendo, upole na maisha ya amani.
Amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya mienendo ya kuchupa mipaka yanawezaka kwa kushikamana na Qur'ani tukufu na suna za Mtume Muhammad (saw) ambaye ametajwa na Qur'ani kuwa ni rehema kwa walimwengu wote.
Sheikh Said Ali Hamduo amezitaka nchi, taasisi za kidini, vituo vya elimu na misikiti kutumia uwezo wao wote kwa ajili ya kupambana na mwenendo wa kuchupa mipaka na utumiaji mabavu. 378064