Muhammad Hussein Safar Harandi ameyasema hayo wakati wa kufunga mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu mjini Tehran na akaongeza kuwa kuwepo kwa wageni hao katika ulimwengu wa Kiislamu ni miongoni mwa matatizo makubwa ya Waislamu.
Waziri wa Utamaduni wa Iran amesema, matatizo mengi yanayotokea kati ya makundi, mataifa na mirengo mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu yanasababishwa na maadui wa dini hiyo.
Amesema kuwa ushirikiano wa baadhi ya nchi za Kiislamu na madola hayo adui ndio tatizo kubwa la ulimwengu wa Kiislamu na akaongeza kuwa wafitini hao wako katika nchi za Kiislamu kwa lengo la kuzusha hitilafu na mifarakano na ndio chanzo cha masaibu ya ulimwengu wa Kiislamu. Amesema kuwa amani na utulivu utarejea katika ulimwengu wa Kiislamu iwapo wafuasi wa dini hiyo watafanikiwa kukata miguu ya maadui wa Uislamu na Mwenyezi Mungu na kuwafukuza katika ardhi zao.
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesisitiza kuwa, miguu ya Marekani na Wazayuni inaonekana mahala popote palipo na fitina na mifarakano katika nchi za Kiislamu. 378382