IQNA

Waislamu wanapaswa kufuata fatuwa za maulamaa katika suala la umoja wa Kiislamu

17:10 - March 18, 2009
Habari ID: 1757502
Hii leo maulamaa wengi wa Kiislamu wanafanya jitihada kubwa za kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu na kwa msingi huo Waislamu wanapaswa kufuata fatuwa zao zinazohimiza umoja na mshikamano.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Ridha Nurullahiyan, Mshauri wa ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambaye ameongeza kuwa mataifa na umma wa Kiislamu unafuata fikra na itikadi za maulamaa kuhusu suala la umoja wa Kiislamu.
Sheikh Nurullahiyan amesema kuwa Waislamu waliowengi wanafuata maulamaa na wasomi wanaoijua dini vizuri ambao daima husisitiza juu ya udharura wa umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Amekosoa misimamo ya makundi yenye misimamo mikali kama Mawahabi na akasisitiza juu ya umuhimu wa kukabiliana nayo.
Amesema kuwa maulamaa wa Kiislamu hawapaswi kunyamaza kimya mbele ya makundi kama hayo kwa sababu Uislamu unapata madhara makubwa kutoka na harakati zao. 378746

captcha