Maulama wa Afghanistan wameyasema hayo katika hafla za kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw). Wamesema kuwa Mtume Muhammad (saw) alikuwa Mtume wa amani, suluhu, upendo na mshikamano.
Maulamaa waliohutubia kikao hicho cha maulidi wamesisitiza kuwa dini ya Kiislamu ina wafuasi katika nchi zote duniani na bado inawavutia wengi katika pande mbalimbali duniani, suala ambalo linatokana na juhudu na sira ya Mtume (saw) na Ahlubaiti zake watoharifu. 378265