Kwa mujibu wa Dakta Yussuf al-Muddalil, Waziri wa Afya wa serikali halali inayoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, idadi hiyo bila shaka itanedelea kuongezeka iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa kwa ajili ya kumaliza mzingiro huo. Ameitaka jamii ya kimatifa kuingilia kati na kuondoa mzingiro huo dhidi ya watu wasio na hatia, na hasa wagonjwa.
Katika kipindi cha mwezi huu wa Machi pekee, zaidi ya wagonjwa 20, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, wamepoteza maisha yao kutokana na mzingiro huo ambao unazuia bidhaa muhumu yakiwemo madawa na vyakula kuingizwa katika Ukanda wa Gaza.
Hivi sasa zaidi ya wagonjwa 1000 wanasubiri kupata idhini ya kutoka katika Ukanda huo ili kwenda kupata matibabu katika mahospitali ya Misri, lakini matumaini yao ya kupata matibabu hayo yanaendelea kudidimia kutokana na hatua ya utawala wa Israel ya kudumisha mzingiro huo na kufunga vivukio vyote vinavyotumika kuingia na kutoka katika ukanda huo kwa ushirikiano wa serikali ya Misri. 380238