Rais Dmitry Medvedev ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Ekmeleddin Ihsanoglu mjini Moscow na kuongeza kuwa Russia ambayo ina jamii za wafuasi wa dini mbalimbali, ina nia ya kustawisha zaidi uhusiano wake na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu katika nyanja mbalimbali.
Medvedev amesisitiza pia juu ya mchango wa Russia wa kustawisha utafiti wa masuala ya Kiislamu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu amesema katika mazungumzo hayo kwamba ulimwengu wa Kiislamu unakaribisha uanachama wa Russia katika jumuiya ya OIC.
Kwa sasa Russia ni mwanachama mtazamaji katika vikao vya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu. 380744