Wakuu na wasimamizi wa vituo vya Qur'ani pamoja na idara mbalimbali za Wizara ya Elimu na Malezi ya eneo hilo walishiriki katika sherehe hizo.
Abdu Aziz Fars, mmoja wa viongozi wa idara za Wizara ya Elimu na Malezi za kaskazini mwa Ukanda wa Gaza amesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa Qur'ani Tukufu ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuzingatiwa maana ya kitabu hicho kitakatifu. Ameongeza kuwa, idara yake imefanikiwa sana katika kuandaa na kusimamia mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kwa wanafunzi na kwamba kufikia sasa idara hiyo imefanya makumi ya wanafunzi kufanikiwa kuhifadhi Qur'ani.
Nuha Shatat, msimamizi mwingine wa masuala ya elimu katika Ukanda wa Gaza pia ameashiria athari za kimaanawi za kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kusema kuwa kujishughulisha na mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu ni moja ya ibada muhimu na bora zaidi ambayo humkurubisha mwanadamu kwa Muumba wake na yenye thawabu nyingi.
Wanafunzi wa kike na kiume walioshiriki katika mashindano hayo walishiriki katika hatua mbalimbali za kuhifadhi Qur'ani Tukufu ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu tatu, juzuu mbili na hatimaye juzuu moja ya kitabu hicho kitakatifu. 381680