Katibu Mkuu huyo wa OIC amezungumza katika kikao hicho cha siku mbili kuhusu 'mchango wa ustaarabu wa Kiislamu na Waislamu katika kubuniwa ustaarabu wa Magharibi.'
Wakati huohuo, hati ya maelewano ya ushirikiano kati ya jumuiya ya OIC na Taasisi ya Muungano wa Staaarabu itatiwa saini mwishoni mwa kikao hicho.
Kikao hicho kinachofanyika kwa wenyeji wa Racep Tayyib Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki, pia kimehudhuriwa na Jose Luis Rodriguez Zapatero, Waziri Mkuu wa Uhispania, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais Barack Obama wa Marekani.
Viongozi na shakhsia wa nchi mbalimbali za dunia akiwemo Muhammad Khatami rais wa zamani wa Iran pia wanashiriki katika kikao hicho.
Muungano wa Staarabu ambao uliasisiwa na Uturuki na Uhispania kwa uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa ulibuniwa mwaka 2005. 383591