IQNA

Fatuwa za fiqhi za Ayatullah Khamenei zatarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili

16:59 - April 07, 2009
Habari ID: 1761679
Fatuwa za kifiqhi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei zimetarjumiwa na zitachapishwa kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
Fatuwa hizo ambazo zimekusanywa na Hujjatul Islam Walmuslimin Mushfiqpour zimetarjumiwa kwa lugha ya Kiswali chini ya usimamizi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania.
Kitabu hicho kimekusanya maswali na majibu ya sheria za fiqhi ya Kiislamu.
Kitabu hicho kimetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili na Bi Maisarah Ali, Katibu wa Taasisi ya al Zahra ya Tanzania.
Kitabu hicho cha fatuwa za Ayatullah Ali Khamenei kina kurasa mia tatu. 383704

captcha