IQNA

Waislamu wa Italia wawasaidia waathirika wa mtetemeko wa ardhi

11:54 - April 09, 2009
Habari ID: 1762314
Waislamu wa Italia wanafanya kila wawezalo ili kuwasaidia wahanga wa mtetemeko wa ardhi wa hivi karibuni katika mji wa L'Aquila makao makuu ya eneo la Abruzzo.
Akinukuu tovuti ya Islamonline, Mustafa Bastanim, Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya eneo hilo amesema kwamba wamepata habari kuwa mahospitali ya eneo hilo yamejaa wagonjwa wanaohitaji damu na kwa hivyo wametoa wito kwa Waislamu kusaidia katika kufidia uhaba wa damu katika mahospitali hayo.
Mustafa Bastanim amesema, Waislamu tayari wameshiriki katika operesheni mbalimbali za kutafuta miili na waathirika wa mtetemeko huo katika vifusi vya majengo yaliyoharibiwa. Bastani ameendelea kusema kuwa hadi sasa hawajafanikiwa kutathmini hasara na maafa yaliyowapata Waislamu wa eneo hilo kutokana na kuharibika kwa mfumo wa mawasiliano katika eneo hilo.
Mtetemeko huo wa ardhi uliokuwa na nguvu ya 6.3 kwa kipimo cha rishta uliotokea siku ya Jumapili, umeuwa zaidi ya watu 270, kujeruhi 1500 na kupelekea wengine 34 kutoweka. 384853
captcha