Kwa mujibu wa gazeti la As-Sharq, mashindano hayo yatawajumuisha wanawake na wanaume katika makundi mbalimbali ya kiumri.
Salim al-Bakri, msimamizi mkuu wa mashindano hayo amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, hadithi zitakazohifadhiwa kwa ajili ya mashindano hayo zimetolewa katika kitabu cha Umdatul Ahkam fi Kalami Kheiril Anam ambacho kimeandikwa na Abdul Ghani al-Maqdisi, mwandishi mashuri wa Kiislamu. Amesema hadithi hizo zimekusanywa katika kijitabu kidogo na kupewa walio na nia ya kushiriki katika mashindano hayo ili kujitayarisha. Kijitabi hicho pia kimesambazwa katika mashule na vituo vya kuhifadhi Qur'ani vinavyosimamiwa na Wizara ya Wakfu ya Qatar.
Al-Bakri amesema kuwa mashindano hayo yataendeshwa na timu ya marefa wenye uzoefu mkubwa kutoka Qatar. Zawadi nono zitatolewa kwa washindi wa mashindano hayo. 384854