Kongamano hilo limeteyarishwa na Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini London na chuo cha Oxford.
Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kuondoa ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu Qur'ani katika dunia ya sasa hususan katika nchi za Magharibi.
Sekretarieti ya kongamano hilo imewataka watafiti na wahakiki kuwasilisha makala zao kuhusu maudhui ya tafsiri ya kisasa ya Qur'ani, tarjumi mpya za Qur'ani, changamoto zinazoikabili Qur'ani katika dunia ya sasa, mawasiliano ya Qur'ani na watu katika karne ya 21, nafasi ya Qur'ani katika mipango ya elimu ya Magharibi, mtazamo wa Qur'ani kuhusu suala la kuheshimu sheria Waislamu aliowachache katika nchi zisizokuwa za Kiislamu, vyombo vya habari duniani na Qur'ani na kadhalika. 385671