Hatua hiyo ilichukuliwa na wawakilishi wa mabunge ya nchi za Kiislamu kama ishara ya kupinga jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.
Wawakilshi wa mabunge ya nchi za Kiislamu walirejea katika kikao hicho baada ya mbunge wa utawala wa Kizayuni wa Israel kukamilisha hotuba yake.
Jumuiya ya Mabunge ya Dunia iliasisiwa mwaka 1889 mjini Geneva Uswisi kwa lengo la kusaidia juhudi za kuimarisha amani na ushirikiano kati ya mataifa mbalimbali kupitia njia ya mazungumzo kati ya mabunge ya dunia.
Mabunge 154 ya nchi mbalimbali duniani ni wanachama katika jumuiya hiyo. 385729