Sheikh Muhammad Hussein amesema kuwa mji mtakatifu wa Quds na msikiti wa al Aqsa vinakabiliwa na hujuma kali ya Israel ya kutaka kuyayahudisha maeneo hayo matukufu na kwamba sasa ni wakati wa Waislamu kutekeleza wajibu wao wa kuyalinda maeneo hayo.
Amesema kuwa maeneo matukufu ya Kiislamu ni amana muhimu kwa Waislamu wote. Ameongeza kuwa Waislamu wote wanapaswa kufanya juhudi za kuulinda msikiti wa al Aqsa na mji wa Quds Tukufu na kuwasaidia wakazi wa eneo hilo. Sheikh Hussein ameashiria mashambulizi makali yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya matukufu ya Kiislamu na akasema kuwa mashambulizi hayo bado yanaendelea na kwamba serikali mpya ya Israel imeendelea kupuuza haki za wananchi wa Palestina. 386091