IQNA

Al-Azhar: Matamshi ya Obama yataimarisha mwenendo wa mazungumzo kati ya Uislamu na Magharibi

16:00 - April 12, 2009
Habari ID: 1763775
Abdul Fatah Alamu al-Jumua, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha al-Azhar amesema kuwa matamshi yaliyotolewa hivi karibuni ya Rais Barack Obama wa Marekani kuhusiana na Uislamu yataimarisha mazungumzo kati ya ulimwengu wa Kiislamu na nchi za Magharibi.
Amesema kwamba matamshi hayo aliyoyatoa katika kikao cha mazungumzo kati ya staarabu nchini Uturuki yanahamasisha mazungumzo kati ya Uislamu na nchi za Magharibi na kwamba yanaonyesha juhudi zake za kuimarisha maisha ya amani yaliyosimama juu ya msingi wa uadilifu na mapambano dhidi ya dhulma na utumiaji mabavu duniani.
Abdul Fatah Alamu al-Jumua amesema, mazungumzo hayo yameondoa mvutano uliokuwepo kati ya nchi za Kiislamu na za Magharibi na kuandaa uwanja wa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya pande mbili hizo.
Amesisitiza kwamba Obama anapasa kutekeleza siasa za aina moja kuhusiana na nchi zote za Kiislamu na kwa msingi wa uadilifu na usawa. Ameendelea kusema kuwa kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu mazungumzo na mataifa mengine na kufanyika juhudi za kuenezwa thamani za kibinadamu ulimwengu ni jambo linalopewa umuhimu mkubwa.
Akizungumza pia katika Bunge la Uturuki, Rais Obama alisisitiza kwamba Marekani haina uadui na ulimwengu wa Kiislamu na kwamba serikali yake inafanya juhudi za kuimarisha mazungumzo ya pande mbili. 386238
captcha