Kwa mujibu wa tovuti ya televisheni ya al-Furat, akizungumza katika marasimu hayo ambayo yaliandaliwa na Taasisi ya Shahid wa Mihrabu katika Chuo Kikuu cha Baghdad, Sayyid Hakim amesema kuwa kutokuwepo Shahid Baqir Sadr katika uwanja wa ulimwengu wa Kiislamu hakujadhuru umoja wa Waislamu na kwamba damu ya shahidi huyo ndiyo iliyopelekea kun'golewa kabisa madarakani kwa serikali ya Saddam Hussein.
Ammar Hakim amesema kuwa ratiba ya utendaji ya Shahid Sadr ilikuwa ikitekelezwa katika mkondo wa ratiba ya umarja wa kidini kwa sababu Shahid Sadr alikuwa amezama katika umarja wa Ayatullah Hakim na Ayatullah Khui. 386398