IQNA

Waislamu kwa mara nyingine tena wanaweza kuwa umma mmoja

13:43 - April 13, 2009
Habari ID: 1764132
Waislamu wanawezakuwa kuwa tena umma mmoja kwa kufuata mafundisho halisi ya dini ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Bernama, maneno hayo yamesemwa na Abdallah Ahmad Badawi, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia ambaye alijiuzulu hivi karibuni, katika sherehe za kumuenzi Mtukufu Mtume (saw) katika Msikiti wa Ijumaa wa mjini Kuala Lumpur. Amesema kuwa katika zama hizi, Waislamu wanakabiliwa na matatizo chungu nzima yakiwemo ya mgawanyiko na hitilafu katika pembe mbalimbali za dunia, jambo ambalo amesema linaweza kutatuliwa kirahisi kwa kufuata mafundisho ya Qur'ani Tukufu na ya Mtume (saw).
Badawi amesema tatizo hilo la kutengana Waislamu lilianza pale Waislamu walipoanza kupuuza mafundisho ya Uislamu ambayo yanasisitiza udugu, usawa, ushirikiano na umoja. Kwa msingi huo, Ahmad Badawi amesisitiza kwamba Waislamu wanapasa kuacha tofauti zao na kutekeleza ipaswavyo majukumu yao ya kuzingatia mafundisho ya Qur'ani na ya Mtume Muhammad (saw). 386770
captcha