IQNA

Makala ya Vita vya Siku 22 vya Israel dhidi Palestina yachapishwa katika jarida la Njia ya Maisha la Senegal

14:49 - April 14, 2009
Habari ID: 1764886
Mkuu wa kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal Muhammad Ali Basiri ameandika makala kuhusu mashambulizi ya siku 22 ya utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Gaza ambayo imechapishwa katika jarida la Njia ya Maisha.
Katika makala hiyo ambayo imebeba kichwa cha maneno kisemacho: Vita vya Siku 22 vya Israel Dhidi ya Wapalestina, Kushindwa au Kushinda? Basiri ameashiria ukatili wa Wazayuni wa Israel huko Gaza na ukatili wa jeshi la utawala huo wakati wa mashambulizi ya siku 33 nchini Lebanon na kubainisha sababu za kushindwa misingi ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi ya Utawala wa Kizayuni wa Israel katika nyanja mbalimbali. Mwandishi huyo ametabiri kwamba utawala bandia wa Israel umo katika hali ya kusambaratika.
Muhammad Ali Basiri ameandika kuwa: Kwa mara ya kwanza kabisa Wapalestina na Walebanon wamefanikiwa kuishinda Israel katika vita vya siku 22 dhidi ya Hamas na mashambulizi ya siku 33 ya utawala huo haramu dhidi ya Hizbullah kwa kutumia aidiolojia ya mapambayo ya Kiislamu iliyotolewa kwenye fikra za hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu). Amesema kuwa aidiolojia hiyo imetoa pigo kubwa la kisiasa, kijeshi na kiuchumi kwa utawala ghasibu wa Tel Aviv.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Senegal amesema kuwa matukio hayo yamebainisha kwamba jeshi la Israel ambalo linadaiwa ni jeshi la nne lenye nguvu kubwa zaidi duniani, limeshindwa na makundi mawili ya Hamas na Hizbullah na hivyo kukadhibisha madai kwamba jeshi hilo halishindiki.
Jarida la Njia ya Maisha hutolewa mara moja kila baada ya wiki mbili mjini Dakar huko Senegal na kusambazwa katika nchi nane za Kiafrika. 387095

captcha