Kwa mujibu wa shirika la habari la Ma'an la Palestina maelfu ya Wapalestina wanaojishughulisha na masuala ya Qur'ani watakusanyika katika makundi ya watu walio na umri wa juu ya miaka 12 kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani katika kipindi cha siku 60.
Kikitoa taarifa kuhusiana na jambo hilo, kituo hicho cha Qur'ani kimesema kuwa wahifadhi Qur'ani 150 na wasimamizi 20 watashiriki vilivyo katika shughuli za kambi hiyo ili kufanikisha malengo yake ya kuhifadhi Qur'ani na kuwalea wahifadhi wapya wa kitabu hicho cha wahyi. Wasimamizi wa mpango huo utakaotekelezwa katika kipindi cha msimu wa joto wamesema kuwa lengo lake ni kunufaika vizuri na kipindi cha mapumziko cha msimu huo na kwamba sharti la kukubaliwa kushiriki ni kuhifadhi kwa uchache juzuu tatu za kitabu hicho cha mbinguni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mpango huo unawajumuisha wanafunzi wa kike na wavulana 1500 katika mkoa wa Rafah pamoja na wanaharakati 10,000 wa mji wa Gaza. 388224