IQNA

Jumuiya ya Vilema wa Kiarabu kuchunguza athari za mashambulio ya Israel Gaza

8:55 - April 15, 2009
Habari ID: 1765109
Jumuiya ya Vilema wa Kiarabu imetangaza kwamba itachunguza athari za mashambulio ya kinyama yaliyotekelezwa hivi karibuni na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na hali ya majeruhi wa mashambulio hayo.
Akizungumza katika makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu huko Cairo Misri, mwakailishi wa jumuiya hiyo ya walemavu wa Kiarabu amesema, ili kufanikisha jambo hilo, jumuiya hiyo ina lengo la kushirikiana na Kamati ya Kuchunguza Jinai za Israel huko Gaza na kuwasilisha ripoti na nyaraka za jinai zilizotekelezwa na utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia kwa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ili kushughulikia hali ya majeruhi wa hujuma hiyo ya kinyama.
Amesema, katika kipindi cha kutekelezwa mashambulio hayo, utawala haramu wa Israel ulikiuka sheria zote za kimataifa kuhusiana na haki za binadamu na hasa kuhusu haki za walemavu ambapo hata ulichukua hatua ya kuwakandamiza na kuwaua kinyama. Amesema kuwa jumuiya yake ina lengo la kuyashinikiza mashirika na jumuiya nyinginezo za kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa ili kuzilazimisha zichukue hatua za dharura za kushughulikia hali ya walemavu wa Ukanda wa Gaza wanaokandamizwa kila uchao na utawala wa Israel usio na huruma wala kuthamini utu wa mtu. 388198
captcha