IQNA

Singapore, mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha huduma za kifedha za Kiislamu

12:10 - April 15, 2009
Habari ID: 1765258
Kikao cha sita cha kimataifa cha huduma za benki ya Kiislamu kitafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao wa Mei nchini Singapore.
Shirika la habari la Bernama limeripoti kuwa kikao hicho kitakachofanyika chini ya anwani ya "Mustakbali wa Huduma za Kifedha za Kiislamu" ni katika jitihada za kujenga mustakbali mzuri kwa ajili ya huduma bora za fedha za Kiislamu.
Mkutano huo ambao utahudhuriwa na wataalamu kutoka Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya, Mashariki ya Kati, kaskazini mwa Afrika na Asia utasimamiwa na Shirika la fedha la Singapore.
Mkutano huo utahutubiwa na Mkuu wa Benki ya Ustawi ya Kiislamu ya Malaysia, Mkuu wa Benki Kuu ya Bahrain, Mwenyekiti wa Shirika la Huduma za Kifedha la Korea Kusini, Mkuu wa Benki Kuu ya Qatar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Fedha ya Saudi Arabia.
Malengo mengine ya kikao hicho yametajwa kuwa ni kutayarisha uwanja mzuri wa kubadilishana uzoefu, mazungumzo kuhusu uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi wa Kiislamu. 388027

captcha