IQNA

Uadui wa Mawahabi dhidi ya Waislamu wa Kishia unahusiana na masuala ya kisiasa

22:48 - April 16, 2009
Habari ID: 1765743
Kundi na Mawahabi linajulikana kote duniani kwa uhasama na uadui wake dhidi ya Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw).
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Najmuddin Tabasi katika kikao kilichojadili nafasi ya Ahlul Bait katika mtazamo wa Mawahabi kilichofanyika katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Sheikh Tabasi amesema kuwa ili kuweza kuelewa vyema mitazamo ya Mawahabi kuhusu Ahlul Bait na wafusi wa madhehebu ya Shia na sababu za uhasama na mwenendo wao mbaya inatupasa kuchunguza historia ya kujitokeza kwa kundi hilo potofu.
Amesema kuwa uhasama wa kundi hilo dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bait unatokana na sababu za kisiasa zisizokuwa na misingi ya mantiki.
Hujjatul Islam Tabasi amesisitiza kuwa kindi la Kiwahabi halina msingi wowote madhubuti wa kiitikadi au kielimu na kwamba Ahlusunna wanatofautiana kikamilifu na kundi hilo.
Amesema kuwa kundi hilo limekuwa likichapisha na kusambaza vitabu vinavyoshambulia na kuchochea fitina dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Ameashiria baadhi ya jinai za kundi hilo na kusema kuwa milipuko ya mabomu inayotokea katika haram na maeneo matakatifu ya Iraq na mauaji ya kinyama ya Waislamu katika maeneo hayo yanatekelezwa na wafuasi wa kundi la Kiwahabi.
Sheikh Tabasi amemalizia kwa kusema kuwa Waislamu wote wa Shia na Suni hawakubaliana na misimamo ya kundi potofu la Kiwahabi. 389058
captcha