Kwa mujibu wa tovuti ya Pkukmweb, kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Kitengo cha Falsafa na Msuala ya Kidini cha chuo kilichotajwa, kitawashirikisha wasomi wengi wa masuala ya sheria, mamufti, washauri wa masuala ya kidini, wakuu wa mashirika ya kifedha na benki za Kiislamu na wanasiasa kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
Masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na masuala ya dini na falsafa ya Kiislamu, maadili ya Kiislamu, Uislamu na sanaa, Uislamu, Qur'ani na hadithi, Uislamu na utambulisho, Uislamu na kumjua mwanadamu, Uislamu na uchumi, Uislamu na siasa, Uislamu na jinsia, Uislamu na sheria, Uislamu na dini nyinginezo na Uislamu na teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kikao cha kwanza kama hicho kilifanyika nchini Malyasia mwaka 2004 ambapo zaidi ya wasomi na wanafikra 200 wa Kiislamu kutoka pande mbalimbali za dunia walishiriki. 389546